Wakati Wa Baraka U Karibu
Wakati wa baraka u karibu,
Utakuwa mchana au usiku;
Arusi ya bibi pamoja na Bwana,
Mfalme wetu tutamwona.
Chorus
Na tutamwona, na tutamwona,
Mfalme wetu tutamwona;
Yuaja tena tutamkaribisha,
Mfalme wetu tutamwona.
U tayari leo akikuita?
Atafurahi nawe kabisa?
Mbinguni ni kwake,
na kwa watu wake,
Mfalme wetu tutamwona.
Ndugu yangu, uwe tayari kwake,
Kumvika taji kichwani pake;
Mfalme za dunia na wainamishwe,
Mfalme wetu tutamwona.
Home