Baragumu Yake Bwana

Baragumu yake
Bwana wakati ikipigwa
Na siku ya milele ikafika;
Hapo waliokombolewa
watakusanyika,
Nitakuwako, jina kuitika.

Chorus
Na majina yaitwapo,
Na majina yaitwapo;
Na majina yaitwapo,
Kuitika jina, nitakuwapo.

Wafu wa Kristo wafufukapo
kwa siku ile
Tutashiriki na fahari yake;
Waliochaguliwa
watakaribishwa kwake,
Nitakuwapo jina kuitika.

Saa zote na tumfanyie
Bwana kazi yake,
Tangu asubuhi hata jioni;
Maisha yetu ikomapo
humu duniani,
Nitakuwako jina kuitika.

Home





Next song