Wamwendea Yesu?
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa,
Na kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Je, neema yake yatumwagiwa?
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
Chorus
Kuoshwa, kwa damu
Itutakasayo ya Kondoo?
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
Wamwandama daima Mkombozi
Na kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa makazi?
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
Atakapokuja Bwana-arusi
Uwe safi kwa damu ya Kondoo
Yafae kwenda mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya Kondoo.
Yatupwe yaliyo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo?
Huoni kijito chatiririka
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo.
Home