Eneza Habari Humu Duniani
Eneza habari humu duniani,
Po pote panapo moyo wa huzuni;
Ndimi za Wakristo zitangaze Neno,
Yupo Mfariji.
Chorus
Yupo Mfariji, Yupo Mfariji,
Roho Mtakatifu, ndiye Msaidizi;
Eneza habari humu duniani,
Yupo Mfariji.
Mfalme wa wafalme, Yesu, umtazame,
Ametuletea siha ya milele;
Mateka wapate Ukombozi wake,
Yupo Mfariji.
Niwezeje mimi kutamka vizuri,
Kumsifu Mwokozi aliye mbinguni?
Nitangaze sasa, neno la furaha,
Yupo Mfariji.
Wenzangu, tuimbe nyimbo za milele:
Mbinguni tujaze na shukrani tele;
Upendo wa Bwana ujulike sana,
Yupo Mfariji.
Home