Imani ya Ajabu Yaufurahisha

Imani ya ajabu
yaufurahisha moyo
Roho akikaa ndani;
Tena, wokovu
utatuletea utakaso
Roho akikaa ndani.

Chorus
Ni Roho Mtakatifu,
Ni Roho Mtakatifu,
Akaapo moyoni,
Twakaa wokovuni.
Ni Roho Mtakatifu.

Hakuna tamaa ya
anasa ulimwenguni
Roho akikaa ndani,
Uovu na dhambi zote
zikachomwa motoni
Roho akikaa ndan. i.

Hatutaanguka tena
bali tutasimania
Roho akikaa ndani,
Hakuna hasira wala
kujipendeza tena
Roho akikaa ndani.

Home