Ushirika Mkuu, Furaha Yangu

Ushirika mkuu, furaha yangu
Kumtegemea Bwana Yesu,
Nina baraka, amani pia,
Kumtegemea Bwana Yesu.

Chorus
Raha, Raha,
Nina raha na salama,
Raha, Raha,
Kwa kumtegemea Yesu.

Ni halisi kutembea naye,
Kwa kumtegemea Yesu.
Naona nuru njiani mwangu,
Kumtegemea Bwana Yesu.

Sioni shaka wala hasara,
Kumtegemea Bwana Yesu;
Nina amani kwake Mwokozi,
Kumtegemea Bwana Yesu.

Home





Next song