Umechoka, Umeshushwa Moyo
Umechoka, umeshushwa moyo?
Mwambie Yesu, mwambie Yesu;
Una huzuni, huna furaha?
Mwambie Yesu sasa.
Chorus
Mwambie Yesu, mwambie Yesu,
Amejulika sana;
Hayuko rafiki kama Yesu,
Mwambie Yesu sasa.
Unalia juu ya haja zako?
Mwambie Yesu, mwambie Yesu;
Mbona wazificha dhambi zako?
Mwanibie Yesu sasa.
Waogopa? Usihuzunike,
MwambieYesu, mwambie Yesu;
Una hofu kwa mambo ya mbele?
Mwambie Yesu sasa.
Waogopa uwazapo kifo?
Mwambie Yesu, mwambie Yesu;
Wautamani ufalme wake?
Mwamble Yesu sasa.
Home