Ukirushwa-Rushwa na Dunia Hii

Ukirushwa-rushwa na dunia hii,
Utakapokufa moyo kwa kudhii,
Zilizo baraka zihesabu tu,
Nawe utaona ni ajabu kuu.

Chorus
Zilizo baraka zihesabu tu,
Mungu aliyofanya ndiyo makuu,
Zilizo baraka zihesabu tu,
Nawe utaona ni ajabu kuu.

Je, unalemewa na mzigo huu,
Msalaba wako ni uzito tu?
Hesabu baraka, moja moja we
Nawe utaimba, usikulemee.

Kwamba huna mali, sifanye tamaa,
Yesu ndiyo mali yako ya kufaa,
Hesabu baraka, za chini na juu,
Hazinunuliki kwa thamani kuu.

Yatuumizayo tuyasahau,
Na baraka zetu tusizidharau,
Hesabu baraka, zisipotee,
Hesabu baraka, hata uzoee.

Haya basi ndugu, twende mbele tu,
Na tusife moyo, Mungu ni mkuu,
Hesabu baraka, nawe mngojee,
Hata mwisho atakuwa na wewe

Home