Kumjia Yesu Mwokozi Wangu
Kumjia Yesu Mwokozi wangu,
Nina Raha, Nina Raha;
Nikiona shida haidhuru,
Ninayo Raha.
chorus
Raha ya ajabu,
Raha yake Mungu;
Tangu mkombozi aliniokoa
Nina Raha.
Amani kama bahari mpana,
Nina Raha, Nina Raha;
Napumzisha roho kwake Bwana,
Ninayo Raha.
Katika rohoni sina vita,
Nina Raha, Nina Raha;
Nimetakaswa, nimeokoka,
Ninayo Raha.
Home
Next song