Mteteeni Yesu

Mteteeni Yesu,
Mlio askari;
Inueni beramu,
Mukae tayari;
Kwenda naye vitani
Sisi hatuchoki
Hata washindwe pia
Yeye amiliki.

Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali;
Leo siku ya Bwana,
Atashinda kweli;
Waume twende naye.
Adui ni wengi,
Lakini kwake Bwana
Tuna nguvu nyingi.

Mteteeni Yesu,
Wenye ushujaa;
Nguvu zenu za mwili
Hazitatufaa;
Silaha ya Injili
Vaeni daima;
Kesheni mkiomba;
Sirudini nyuma.

Mteteeni Yesu,
Vita ni vikali,
Wengi wamdharau,
Hawamkubali;
Ila atamiliki
Tusitie shaka;
Kuwa naye vitani
Twashinda hakika.

Home





Next song