Kutakuwa Mwanga
Kutakuwa mwanga nyumbani
mwa Bwana,
Nifikapo mwisho wa mwendo;
Nitapata raha mkononi mwa
Bwana,
Nifikapo mwisho wa mwendo.
chorus
Safari ikomapo siku ya mwisho,
Nitakaribishwa na pendo;
Kwa kuwa Mwokozi ananingojea,
Nifikapo mwisho wa mwendo.
Sitazikumbuka taabu za njia,
Nifikapo mwisho wa mwendo;
Sitawakumbuka walionipinga,
Nifikapo mwisho wa mwendo.
Nimwone Rafiki aliye Mwokozi,
Nifikapo mwisho wa mwendo;
Hiyo natamani katika mbinguni,
Nifikapo mwisho wa mwendo.
Home