Mikononi Mwa Yesu

Mikononi mwa Yesu,
Kifuani mwake,
Mapenzi yanilinda
Sina hofu kamwe;
Asha tuma wajumbe
Kuleta habari,
Ya kutufurahisha
Katika safari;

chorus
Mikononi mwa Yesu,
Kifuani mwake,
Mapenzi yanilinda
Sina hofu kamwe.

Mikononi mwa Yesu,
Tashwishi sinayo;
Maonjo hayadhuru,
Madhambi hayamo.
Nikiwa na Mwokozi
Sioni majonzi;
Mashaka ni machache,
Machache machozi. ;

Yesu, Mwokozi wangu
Akafa Mtini;
Yesu, Mwamba wa Kale
Namtumaini,
Namngojea Bwana,
Mchunga, Rafiki,
Hata kupambauka,
Huko mashariki.

Home





Next song