Kwa Damu ya Yesu Naokoka

Kwa damu ya Yesu naokoka!
Nikageuka niwe mtu mpya;
Baba asifiwe na Mwana pia,
Kwa damu ya Yesu naokoka.

chorus
Naokoka! Naokoka!
Dhambi zangu zote zaondolewa;
Naokoka! Naokoka!
Naokolewa na damu yake Bwana.

Kwa damu ya Yesu naokoka!
Malaika wafurahi kuona;
Ni mwana wa Baba mrithi na Mwana,
Kwa damu ya Yesu naokoka.

Kwa damu ya Yesu naokoka!
Mapenzi ya Baba yametendeka;
Alininunua na gharama kubwa.
Kwa damu ya Yesu naokoka.

Kwa damu ya Yesu naokoka,
Asifiwe Baba na Mwana pia;
Roho asifiwe huleta raha,
Kwa damu ya Yesu naokoka.

Home