Nitaiimba Hadithi
Nitaimba hadithi,
Juu ya Yesu Mwokozi;
Aliyetoka mbinguni
Kunifia Kalvari.
chorus
Ndiyo nitaimba hadithi
Juu ya Mwokozi Yesu,
Alinifia rnsalabani,
Nimwirnbie kumsifu.
Nilipotelea mbali,
Yesu akanipata;
Na alinikumbatia,
Kwake akanivuta.
Nilijeruhiwa sana,
Nikaponywa na Bwana;
Kama kipofu nikawa,
Akaniponya tena.
Giza imenizunguka,
Huzuni hunipata;
Bali Mwokozi yu nami,
Kwa mkono hunishika.
Atanilinda kabisa
Hata mwisho wa siku,
Na atanikaribisha
Kufika kwake mbingu.
Home