Vita Vya Ukombozi

Vita vya ukombozi, vilianzishwa
Mji mtakatifu makao ya Bwana
Dhambi ilipoingia kwa ibilisi
Majeshi takatifu walimshinda

Na sisi tutashinda
Kwa damu ya Mwana
Kondoo na kwa neno la,
Ushuhuda wetu

Pale msalabani tuliwezeshwa
Kumshinda shetani, dhambi na mauti
Tena hatutapenda maisha yetu
Tutakubali kuyapoteza vitani

Vita vya ukombozi
Alivishinda
Juu ya msalaba, Yesu Mwokozi
Alitoa tangazo
Yenye ushindi
Hapo aliposema, yote yamekwisha

Vita vya ukombozi
Walivipata
Manabii na mitume, na walimshinda
Mnyama kwa damu ya,
Mwana Kondoo
Na kwa ushuhuda wao mpaka walilala

Vita vya ukombozi
Vya mwana damu
Kati ya Mwana Kondoo
Na mwovu shetani
Vilikuwa vikali
Msalabani
Dunia pia mbingu, vikishuhudia

Njia ya Kalvari
Alikanyanga
Kusudi wewe nami
Tupate wokovu
Mbona wadanganyika,
Unachelewa,
Vita vimetangazwa
Vya mwana adamu

Home





Next song