Yesu Unihifadhi
Yesu unihifadhi
Hapa Msalabani;
Wajiao Kalvari,
Waponywe damuni.
Chorus
Msalaba, Msalaba,
Humu nina sifa;
Hata nitapumzika,
Mahali pa raha.
Karibu na Msalaba
Nimepatikana,
Na pendo na neema
Nimezungukiwa.
Karibu na Msalaba,
Na Mwana wa Mungu;
Nitatembea naye,
Aliye Mtukufu.
Karibu na Msalaba
Nitakesha sana;
Hata nitawasili
Mbinguni kukaa.
Home