Ni Tamu Kumjua Yesu

Ni tamu kumjua Yesu,
Na kumwamini pia;
Kutegemea ahadi
Ni sahihi kabisa.

Chorus
Yesu, Yesu, namwamini,
Nikamthibitisha;
Yesu, Yesu, wa thamani,
Nizidishwe kumjua.

Ni tamu kumjua Yesu,
Kumwamini kabisa;
Nizame damuni mwake,
Damu ya kutakasa.

Ni tamu kumjua Yesu,
Na kuziacha dhambi;
Kupokea kwake Yesu
Uzima na amani.

Nina furaha kumjua
Mwokozi na Rafiki;
Yeye Yu nami daima
Katika maishani.

Home





Next song