Bwana Nieleze

Bwana nieleze kile kilicho
kufanya ukaja hapa wakati ule
Yote ya mbinguni hukuyaona kitu,
ukaja ishi na viumbe vyako,

Hebu nieleze kwa sauti ya upole,
akili zangu bwana Ni fupi,
rudia rudia kama vile kwa mtoto,
nisisahau hata kidogo

Walipo kusulubisha msalabani
hakuna aliye kusaidia
Ukafa kifo cha uchungu na Aibu
Kwa dhambi iliyokua yangu

Zidi kunionyesha ubaya wa dhambi
Najua ndio iliyokuua
Na nigeukapo bwana kutenda dhambi
Bwana nirudi kwa fimbo yako

Home





Next song