Aniongoza Popote
Aniongoza popote,
Nimwandame siku zote;
Kwa ajili yangu mimi,
Aliuawa Kalvari.
Chorus
Nitaongozwa na Bwana,
Usiku kucha na mchana;
Yesu Rafiki wa heri,
Ninakumbuka Kalvari.
Lanitosha Neno lake,
Nishikwe na mkono wake;
Mapenzi yake ni heri,
Yalitimizwa Kalvari.
Nitaendelea mbele,
Pamoja naye milele;
Pendo lake ni hiari,
Bwana Yesu wa Kalvari.
Home