Aitwa "Wa Simanzi."
Aitwa "Wa Simanzi,"
Mwana wa Mwenye enzi
Mwenye mengi mapenzi!
Nasifiwe Bwana Yesu.
Akawa matesoni
"Mungu Mwana" yakini
Akatoka mbinguni
Nasifiwe Bwana Yesu.
Akapata dhihaka
Mzoea-mashaka
Ndiye yetu sadaka:
Nasifiwe Bwana Yesu.
Tu wenye dhambi sana,
Kwake dhambi hamna:
Na Mungu twapatana:
Nasifiwe Bwana Yesu.
Alikufa Mtini
Akalia dhikini
Sasa yuko mbinguni:
Nasifiwe Bwana Yesu.
Punde atarejea
Yesu kutunyakua
Ndipo tutamwimbia,
Nasifiwe Bwana Yesu."
Home