Ni Tabibu Wa Karibu

Ni Tabibu wa karibu,
Tabibu wa ajabu;
Na rehema za daima,
Ni dawa yake njema.

Chorus
Imbeni, malaika,
Sifa za Yesu Bwana;
Pweke limetukuka
Jina lake Yesu.

Hatufai kuwa hai,
Wala hatutumai;
Ila yeye kweli ndiye
Atupumzishaye.

Dhambi pia na hatia
Ametuchukulia;
Twenendeni na amani
Hata kwake Mbinguni.

Huliona tamu jina
La Yesu Kristo Bwana;
Yuna sifa mwenye kufa
Asishindwe na kufa.

Kila mume asimame,
Sifa zake zivume;
Wanawake na washike
Kusifu jina lake.

Na vijana wote tena,
Wampendao sana
Waje kwake, wawe wake
Kwa utumishi wake.

Home





Next song