Jua Kila Ling'arapo
Jua kila ling'arapo
Yesu atashinda huko
Mfalme wa nchi zote,
Hata dunia iishe.
Na daima aombewe,
Atawazwe na majurnbe,
Kama udi Jina lake
Na sadaka tupeleke.
Kila lugha na taifa
Watamwimbia na sifa,
Na Jina lake vijana
Vitalitukuza sana.
Ashindapo ni furaha
Kwa waovu msamaha;
Huacha huru wafungwa,
Wahitaji hushibishwa.
Watu wote na wasifu,
Wampe na utukufu;
Malaika, watu nao
Wamwimbie sifa zao.
Home