Umesoma Hadithi ya Yesu?

Umesoma hadithi ya Yesu?
Alisulibishwa;
Deni yako hapo ililipwa
Na damu, kuokoa.

Chorus
Yesu alikuvunjikia,
Akafa kukufidia;
Pendo lake ndilo La ajabu,
Alikuvunjikia.

Taji ya miiba iliwekwa
Kichwani mwa Bwana;
Kwa adui aliwaombea
Wawe na masamaha.

Umesoma habari ya mwivi
Aliyeangikwa?
Na jinsi alivyomwomba
Na kufarijiwa?

Wajua ya kwamba kifoni
Kapaza sauti?
Akasema kwamba imekwisha
Upate kuokoka.

Home