Peleleza Ndani Yangu

Peleleza ndani yangu,
Iwe safi nia,
Kwangu kama kwako Mungu,
Idhihiri pia.

Peleleza moyo wangu
Unifunulie,
Yaliyomo ndani yangu
Nami niyajue.

Kwanza washe zako tambi,
Kumefunga giza;
Nijue ambavyo dhambi
Ni la kuchukiza.

Peleleza na mawazo,
Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo,
Maumbuo-umbo.

Zidi kuyapeleza
Katikati yangu
Hata wishie nifundisha
Udhaifu wangu.

Hapo nikikwinamia
Mbele zako, Mungu,
Hakika nitakujua
U Mpenzi wangu.

Home