Mwokozi Alinifia

Mwokozi alinifia,
Yesu Mfalme wangu;
Akajitoa kabisa,
Kwa niaba yangu.

Chorus
Mwokozi, nisaidie,
Niwe mwaminifu;
Utakapomiliki juu,
Bwana, nikumbuke.

Aliugua mtini,
Kwa maovu yote;
Alikufa hapa chini,
Tuokoke sote.

Nijifiche uso wangu,
Nione msalaba;
Nimpe shukrani yangu,
Astahili sifa.

Sina uweza kulipa,
Deni ya upendo;
Bali Yesu, najitoa,
Nitumike kwako.

Home





Next song