Uniumegee Mkate Hal

Uniumegee Mkate Hai,
Kama ulivyomega zamani,
Ninakutafuta, Ewe Bwana,
Roho yangu yakutaka sana.

Nitashinda Bwana nitashinda
Kama wewe pia ulishinda
Nitapitia mapitioni mwako
Nimeanza Bwana nitashinda

Uniumegee Mkate Hai,
Neno lako likae moyoni;
Mawazo ya ndani yawe safi,
Niongozwe daima, Mwokozi.

Neno lako Bwana, nilione,
Ujumbe wako niandikie;
Tushirikiane na upendo,
Uniitilie sura yako.

Home





Next song