Baba Yetu Aliye Mblnguni
Baba yetu aliye mbinguni
Amenifurahisha yakini
Kuniambia mwake Chuoni
Ya kuwa nami Yesu pendoni.
Chorus
Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda, Anipenda:
Anipenda Mwokozi Yesu,
Anipenda mimi.
Nimuachapo kutanga mbali
Yeye yu vivyo, hupenda kweli,
Hunirejeza kwake moyoni:
Kweli yu nami Yesu pendoni.
Anipenda! Nami nampenda;
Kwa wokovu alionitenda:
Akanifia Msalabani
Kwa kuwa nami Yesu pendoni.
Haya kujua yanipa raha;
Kumuamini kuna furaha:
Humfukuza mara Shetani,
Kwona yu nami Yesu pendoni.
Sifa ni nyingi asifiwazo,
Moja ni sana katika hizo,
Wala siachi, hata mbinguni,
Kwimba, "Yu nami Yesu pendoni."
Home
Next song