Sijui Ilipotoka

Sijui ilipotoka,
Amani moyoni;
Bali najua najazwa
Na raha moyoni.

Chorus
Ni amani moyoni mwangu,
Ni amani moyoni mwangu;
Ijapo dhambi ziko karibu,
Kristo Yuko, Hudumu.

Kwa mambo ya maishani
Sitafadhaika,
Nikilemewa kazini
Sitahuzunika.

Sijui juu ya upendo
Jinsi ukuwavyo,
Umenifufusha roho
Kufurahi nao.

Sistahili kifo chake
Wala ukombozi,
Ningeteswa hapa naye,
Naye ningerithi.

Home





Next song