Wachunga Walipolinda
Wachunga walipolinda
Kucha nyama zao,
Malaika mtukufu
Alishuka kwao.
Wakacha sana wachunga,
Akawatuliza,
"Nawaletea habari
Ya kuwapendeza.
"Mji ule wa Daudi
Leo amezawa
Mwokozi, ni Kristo Bwana,
Ilivyoandikwa:
"Huyo Mwana wa mbinguni
Ataonekana,
Amelazwa kihorini
Malazi hapana."
Alipokwisha yanena
Malaika hao
Waliimba wimbo huu,
Usio na mwisho:
"Enzi ni yake Mungu juu.
Na nchi salama,
Kwa watu nao radhi kuu,
Sasa na daima."
Home
Next song