Sioni Haya kwa Bwana
Sioni haya kwa Bwana
Kwake nitang'ara!
Mti wake sitakana
Ni neno imara!
Chorus
Msalaba ndio asili ya mema,
Nikatua mzigo hapo:
Nina uzima, furaha daima
Njooni kafurahini papo.
Kama Kiti chake vivyo
Ni yake ahadi:
Alivyowekewa navyo
Kamwe havirudi.
Bwana wangu, tena Mungu
Ndilo lake jina!
Hataacha roho yangu
Wala kunikana.
Atakiri langu jina
Mbele za Babaye:
Anipe pahali tena
Mbinguni nikae.
Home
Next song