Kibarikiwe Kifungo

Kibarikiwe kifungo
Kitufungiacho mioyo,
Ushirika wetu wa fikira zetu
Ni kama ule wa mbingu.

Mbele ya enzi ya Baba,
Dua zetu twaziomba;
Hofu zetu na matumaini yetu,
Hayo ni mamoja kwetu.

Huzuni zetu twashika,
Na mizigo yetu pia;
Ndani yao yote twashirikiana
Hata katika kulia.

Tutawanyikapo mbali,
Hiyo yatufadhaisha;
Lakini tungali pamoja rohoni
Hata tutakutanika.

Home





Next song