Yesu Uniongoze

Yesu uniongoze,
Juu ya bahari yote;
Kwelea na mawimbi,
Nisizame majini,
Dira yako nipate,
Yesu uniongoze.

Kwa bahari waweza,
Maji yake kushinda;
Mawimbi yasikia
Usemapo, "Tulia;"
Bwana wa bahari Ewe,
Yesu, uniongoze.

Nifikapo ardhini
Kwa kuvuka kilindi,
Nitapata pumziko
Kutegemea kwako;
Uniambie tena,
"Ndiyo, nitaongoza."

Home





Next song