Neema ya Mpendwa Bwana
Neema ya Mpendwa Bwana,
Neema ishindayo dhambi;
Pa Kalvari akamwaga damu,
Damu yake Mwana wa Mungu.
Chorus
Ni neema, ni neema,
Neema iliyotakasa;
Ni neema, ni neema,
Neema ishindayo kosa.
Dhambi ni kama dhoruba kuu,
Iletayo hasara kwetu;
Bali Yesu ana neema,
Iuonyeshayo Msalaba.
Hatuwezi dhambi kuficha,
Tupateje kutuosha?
Tazameni damu ya Bwana,.
Hiyo yafaa kutakasa.
Kweli neema ya ajabu
Yawajia waaminio;
Watakao kumwona Yesu,
Pokeeni neema hiyo.
Home
Next song