Nikimaliza Kazi ya Maishani

Nikimaliza kazi ya maishani mwangu,
Nitaacha dunia kwa salama;
Nitamjua Mwokozi, nikifika huko juu,
Atanikaribisha kwa furaha.

Chorus
Nitamjua, nitamjua,
Nikisimama karibu kwake;
Nitamjua, nitamjua,
Kwa makovu mikononi mwake.

Mle mbinguni nitamshangilia Mwokozi
Nikimwona Yesu uso kwa uso;
Amestahili sifa, aliye Mkombozi,
Amenipa rehema na upendo.

Nitaona wale walionitangulia,
Waniashiria niende pale;
Nitafurahi nao nitakapoingia,
Bali mwanzoni, Mwokozi nimwone.

Nikifika nitavikwa mavazi meupe,
Sitaona huzuni pale, kamwe;
Kwa furaha nitaimba wimbo wa milele
Bali mwanzoni, Mwokozi nimwone.

Home





Next song