Nafurahi Moyoni Mwangu
Nafurahi'moyoni mwangu,
Yesu ameniambia,
"Tulia, usiwe na hofu
Mwendoni mwa maisha."
Chorus
Yesu, Yesu, Yesu,
Ni jina tamu;
Limeniridhisha,
Katika mwendo wangu.
Kwa uovu nilianguka,
Katika maisha yangu;
Bali Yesu akanivuta,
Yeye Mwokozi wangu.
Naishi kwa upendo wake,
Kweli, amenipumzisha
Nikimtazama uso wake,
Atanisalimisha.
Nikihangaika njiani,
Yesu ataniongoza;
Amenitolea ahadi,
Uchungu atapoza.
Atarudi kutoka mbingu,
Ili anikaribishe,.
Na tutapita kwa mawingu,
Ataniwasilisha.
Home