Wautafuta Ujazo Wa Baraka

Wautafuta ujazo
wa baraka ya Bwana,
Moyoni mwako leo?
Kwa jinsi Baba asemavyo
pokea ahadi
Utapata baraka.

Chorus
Atakujaza kabisa moyo wako,
Kama alivyosema,
vyombo vyako ataka
Atakujaza kabisa moyo wako
Na Roho Mtakatifu.

Vileteni vyombo
vilivyotakaswa na damu
Njoni, mliotaka;
Kwa unyenyekevu
jitoeni mbele za Mungu
Hata kuja kwa Roho.

Neema ya Bwana Yesu,
haipunguki kamwe
Wala upendo wake;
Kwa kadiri ya ahadi
yake atakijaza
Kila chombo na Roho.

Home





Next song