Yuko Mwokozi Wa Ajabu
Yuko Mwokozi wa ajabu,
Alinifia mtini;
Na alitumwagia damu,
Tuokoke, wenye dhambi.
chorus
Alinisulibishiwa
Alinisulibishiwa;
Akafa mtini pa Kalvari,
Alinisulibishiwa.
Alitoka kwake mbinguni,
Mapenzi ayatimize;
Akazaliwa na bikira,
Mfano wa mtu avikwe.
Akapigwa kwa dhambi zetu,
Akachukua taabu;
Yu Mpozi wa ugonjwa wetu,
Hayo alifanya kwetu.
Kwa wengine akajitoa,
Alipoondoa dhambi;
Makao atutayarisha,
Tuingie mbinguni.
Home