Nishike Mkono

Safari ya imani nakutazama Yesu
Nataka nifike ng'ambo salama
Lakini njiani mawimbi ni mengi
Mashaka yanisonga kuniangamiza

Nishike mkono nisizame
Mawimbi ni mengi niokoe

Mawimbi ni makali nahitaji msaada
Nishike mwokozi niwe salama
Wewe uliyeniita nakuja kwa neno lako
Napata kutembea kwa neno lako

Safari ya imani natembea kwa imani
Dhambi isinishinde nisaidie
Katika majaribu makali Kama moto
Najua nitatoka kama dhahabu

Home





Next song