Uje Unisaidie
Uje unisaidie,
Mwokozi wa Baraka;
Rehema yako ni tele,
Nikutolea sifa:
Unifundishe kusifu,
Sifa za malaika;
Nimekaa upendoni,
Upendo wa hakika.
Naja kwako unishike,
Najitoa kabisa;
Kwa mapenzi yako niwe.
Mwaminifu wa sifa:
Nilipotembea mbali,
Yesu alinipata;
Akaniokoa kweli,
Kwa damu ya salama.
Kwako nimekuwa mdeni,
Umenipa neema;
Nisipotelee mbali,
Unifunge kwa wema:
Ni mwenye kutangatanga,
Ni mwenye kupotea:
Uchukue moyo wangu,
Unifunge kabisa.
Home