Muda Mwingi Nilipotea
Muda mwingi nilipotea,
Sikufahamu Msalaba;
Wala aliyenifilia,
Kwa Kalvari.
Rehema bure na neema.
Samaha nalo nilipewa;
Ndipo aliponifungua,
Kwa Kalvari.
Kwa Neno lake Bwana Mungu,
Nilijiona mimi mwovu;
Nikageuka na kutubu,
Kwa Kalvari.
Yote kwa Yesu namtolea,
Ndiye Mfalme wa pekee sasa;
Kwa furaha nitamwimbia,
Kwa Kalvari.
Jinsi pendo lilivyo kuu,
Neema ilishushwa toka juu,
Alitufanyia wokovu,
Kwa Kalvari.
Home