Dhambi Ikikulemea

Dhambi ikikulemea,
Kwa Bwana rehema:
Hivi sasa tegemea
Neno la salama.

Chorus
Tegemea, tegemea,
akwita sasa.
Ni Mwokozi, ni Mwokozi;
amini sasa.

Yesu amemwaga darnu
Ya nyingi baraka:
Nawe sasa oga mumu
Zioshwamo taka.

Ni njia Yeye hakika
Hwongoza rahani:
Usikawe kumshika.
Uwe barakani.

Karibu nawe wingie
Mwetu safarini,
Twende tukamwamkie,
Milele Mbinguni.

Home





Next song