Furaha kwa Ulimwengu

Furaha kwa ulimwengu!
Bwana arnekuja;
Nyote mkaribisheni,
Mioyo yenu na mpeni;
Wote wamshangilie,
Wote wamshangilie,
Na wote, na wote wamshangilie.

Furaha kwake dunia
Mwokozi ni Mfalrne;
Bonde na mlima na mwamba,
Maji mitoni na shamba,
Rudisheni sauti,
Rudisheni sauti,
Rudisheni, na rudisheni sauti

Dhambi zisiongezeke,
Wala wahalifu;
Yuaja kutubariki,
Atuletea ushindi;
Kuhanibu dhambi,
Kuharibu dhambi,
Na kuharibu, na kuharibu dhambi

Atawala na neema,
Kwao mataifa;
Utukufu na waone,
Haki yake itendeke;
Kwa upendo wake,
Kwa upendo wake,
Kwa upendo, na kwa upendo wake.

Home





Next song