Mwokozi Wetu Utuongoze
Mwokozi wetu utuongoze,
Twakuhitaji sana;
Na malisho yako utulishe,
Tukae na salama.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Sisi tu mali zako;
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Sisi tu mali zako.
Bwana ututendee hisani,
Mlinzi wetu na uwe;
Na utuhifadhi maishani,
Tusipotee kamwe.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Utusikie sasa;
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Utusikie sasa.
Umeahidi kutupokea,
Ijapo tu maskini,
Una rehema kututuliza,
Na nguvu ya ushindi.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Tugeuke mapema,
Bwana Yesu, Bwana Yesu
Tugeuke mapema.
Tuitafute kibali yako,
Kuitenda mapema;
Bwana na Mwokozi peke yako,
Utujaze na mema.
Bwana Yesu, Bwana Yesu,
Utupende daima
Bwana Yesu, Bwana,
Utupende daima.
Home