Niilipoona Chemchemi

Nilipoona chemchemi,
Kwa dhambi zangu zote;
Nikasikia sauti
Kusema, "Uwe safi."

Nitamsifu, nitamsifu,
Msifuni Mwana-Kondoo;
Mpeni sifa za moyo,
Kwani hutupa utakaso.

Njia yake ni nyembamba,
Vyote namtolea;
Fahari na tumaini,
Hayo nimeondoa.

Moyo wangu ulichomwa,
Kwa moto wake Mungu;
Sitakosa kumsifu,
Bwana wa utukufu.

Jina la Yesu ni heri,
Aliyenikubali;
Amezisamehe dhambi,
Tena hunifadhili.

Utukufu kwake Baba,
Utukufu kwa Mwana;
Utukufu naye Roho,
Utatu ndani Mmoja.

Home





Next song