Huniongoza Mwokozi

Huniongoza Mwokozi,
Ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo,
Ataniongoza papo.

Chorus
Kuongoza hunishika;
Kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye
Kristo aniongozaye.

Pengine ni mashakani
Nami pengine rahani;
Ni radhi, ijayo yote,
Yupo nami siku zote.

Mkono akinishika
Kamwe sitanung'unika:
Atakachoniletea
Ni tayari kupokea.

Nikiisha kazi chini
Takwenda huko mbinguni,
Nako nitamtukuza
Kristo aliyeongoza.

Home





Next song