Nasikia Kwitwa
Nasikia kwitwa
Na sauti yako
Nikasafiwe kwa damu
Ya kwangikwa kwako.
Chorus
Nimesongea Mtini pako,
Unisafi kwa damu
Ya kwangikwa kwako.
Ni mnyonge kweli,
Umenipa nguvu
Ulivyonisafi taka
Ni utimilivu.
Yesu hunijuvya:
Mapenzi imani,
Tumai, amani, radhi,
Hapa na mbinguni.
Huipa imara
Kazi yake, ndani:
Huongezeka neema,
Ashindwe Shetani.
Huishuhudia
Mioyo ya imani
Ya kuzipata ahadi
Wakimuamini.
Napata wokovu
Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu
Na haki daima.
Home