Nitaonana na Yesu
Nitaonana na Yesu,
Uso kwa uso kweli;
Siku ile shangwe tele,
Nikimwona Mwokozi.
Chorus
Tutaonana na macho,
Huko kwetu Mbinguni;
Na kwa utukufu wake,
Nitamwona milele.
Sasa siwezi kujua
Jinsi alivyo hasa;
Bali atakapokuja,
Nitamwona halisi.
Mbele yake yafukuzwa
Machozi na huzuni:
Kipotovu kitanyoshwa,
Fumbo litafumbuka.
Uso kwa uso! Hakika
Pale pale furaha;
Nitafurahi kabisa,
Nikimwona Mwokozi.
Home