Katika Gethsemane Yesu Aliteswa

Katika Gethsemane Yesu aliteswa,
Kikombe chenye huzuni, hapo alikunywa;
Pa Kalvari, Msalaba aliuchukua,
Alitenda mapenzi ya Baba.

chorus
Pekee, ndiyo pekee, Yesu alikufa,
Pekee, ndiyo pekee alinifungua;
Dunia hii iliaibishwa hata Yesu
Alitenda mapenzi ya Baba.

Yesu alikubali kunifia mtini,
Akamwaga damu yake nisife dhambini;
Akawekwa katika kaburini mwambani,
Alitenda mapenzi ya Baba.

Alifufuka kutoka kifo na kaburi,
Akawa Mshindi juu ya mauti na dhambi;
Akaniokoa nisiende hukumuni,
Alitenda mapenzi ya Baba.

Home





Next song