Mungu Wangu, Ndiye na Mwamini

Mungu wangu, ndiye
namwamini,
Po pote nilipo duniani;
Lo lote lanijialo,
Baba yangu hunitunza humo.

chorus
Namwamini Mungu hunipenda
Katika dhiki ama mashaka;
Matesoni hunilinda,
Baba yangu hunitunza sana.

Mungu hulinda viumbe vyake,
Huviongoza njiani mwake;
Najua anikumbuka,
Baba yangu hunitunza sana.

Njia ijapokuwa gizani,
Kondoo hawasahauliwi;
Mungu Mchunga aongoza
Baba yangu hunitunza sana.

Home





Next song