Najua Jina Niliheshimulo

Najua jina niliheshimulo,
Lanipendeza rohoni mwangu;
Jina thamani kupita hesabu,
Yesu ndilo jina la ajabu.

chorus
Moyo wangu umependezwa sana,
Nikumbukapo jina la Kristo;
Sina jina jingine liwezalo,
Kunipatia wokovu nalo.

Jina hilo huniletea raha,
Huondoa sikitiko langu;
Huimarisha aliyelemewa,
Jina hilo huponya kabisa.

Jina hilo litadumu milele.
Nguvu zake hazibadibiki;
Jina hilo litang'ara daima,
Jina la Yesu halipunguki.

Home





Next song